Mialiko ya Kidigitali Yenye Udhibiti wa Kuingia

Shiriki Matukio Maalum
kwa RSVP na Check-in

Tengeneza kadi nzuri za matukio, kusanya majibu ya RSVP, tuma QR za wageni, na simamia check-in mlangoni pamoja na fedha za tukio sehemu moja.

0+Violezo
RSVP + QRMtiririko Mmoja
Kuingia MlangoniTayari
Birthday
Heri ya Birthday!
Sendoff
Safari Njema
Harusi
Upendo wa Milele

Tunakutakia maisha ya furaha na upendo pamoja.

Inavyofanya Kazi

Buni mara moja. Shiriki popote. Scan wageni.

Kutoka kutengeneza kadi hadi RSVP, utumaji, QR ya kuingia, na ufuatiliaji wa michango katika mtiririko mmoja

01

Chagua Kiolezo

Chagua kutoka kwenye mkusanyiko wa violezo vilivyosanifiwa kitaalamu kwa kila tukio.

02

Binafsisha

Hariri maudhui, rangi, fonti, na picha mpaka kadi iwe kama unavyotaka.

03

Tuma na RSVP + QR

Tuma kwa WhatsApp au SMS, ambatanisha QR za kuingia kwa kila mpokeaji, na kusanya majibu ya RSVP.

04

Fuatilia Kuingia na Fedha

Ona check-in, shughuli za scanner, majibu ya RSVP, mipango ya michango, bajeti, na exports kutoka Mialiko Yangu.

Udhibiti wa Kuingia

QR za mlangoni na RSVP zipo ndani ya mtiririko wa mwaliko

Kwa Wedding na Sendoff, wageni wanaweza kupokea QR ya kuscan wakati wa kutuma mwaliko. Mwenye tukio anaweza kushiriki link za scanner kwa watu wa mlangoni na kuona logi za check-in baadaye.

Link za RSVP za wote

Shiriki ukurasa mmoja wa mwaliko ambapo wageni huandika jina, simu, jibu, na ujumbe.

QR za kila mgeni

Tengeneza ruhusa za single, double, custom, au open entry kwa wapokeaji wakati wa dispatch.

Scanner za mlangoni

Ruhusu watu wa kuaminika wascan bila kuingia akaunti, zikiwa na muda wa kuisha, kuzimwa, na kikomo cha scan.

Ripoti za check-in

Pitia wageni waliokuwa scanned, shughuli za RSVP, ripoti zilizopakuliwa, na takwimu za kuingia.

Mipango Iliyounganishwa

Mialiko na fedha za tukio sasa zinafanya kazi pamoja

Baada ya kuhifadhi kadi, unaweza kuiunganisha na mpango wa michango, kuona waliolipa, na kujua kama bajeti ya tukio bado iko sawa.

Wachangiaji

Fuatilia familia, marafiki, na ndugu

Ona nani amelipa yote, nani analipa kidogo kidogo, na nani bado ana ahadi.

Bajeti

Angalia salio halisi la tukio

Linganisha michango iliyokusanywa na makundi ya bajeti pamoja na matumizi yaliyoandikwa.

Vidokezo

Jua cha kufuatilia baadaye

Tumia vikumbusho, viashiria vya maendeleo, na mapendekezo rahisi kabla ya kuzidisha matumizi.

Uko tayari kuendesha mwaliko wa tukio sehemu moja?

Buni kadi, shiriki link ya RSVP, tuma QR za wageni, scan mlangoni, na simamia fedha kwa urahisi.