Masharti ya Huduma
Masharti ya Sayari E-card
Masharti haya yanaeleza jinsi Sayari E-card inavyoweza kutumika kutengeneza, kushiriki, kusimamia, na kufuatilia mialiko ya kidigitali, majibu ya RSVP, QR za kuingia kwa wageni, na ripoti za tukio.
1. Kutumia Sayari E-card
Unaweza kutumia Sayari E-card kwa matukio ambayo una mamlaka ya kuyaandaa au kuyasaidia. Unawajibika kwa maudhui ya mwaliko unayotengeneza, wapokeaji unaowasiliana nao, na taarifa za wageni unazopakia au kukusanya.
2. Akaunti na Ufikiaji
Unawajibika kulinda taarifa zako za kuingia. Ikiwa akaunti yako itatumika kutengeneza kadi, kutuma dispatch, kusimamia link za RSVP, kuidhinisha violezo, au kuscan wageni, tutachukulia vitendo hivyo vimefanywa na wewe au mtu uliyemruhusu.
Ukiwaalika wafanyakazi, designers, au wascanaji wa mlangoni, mpe ufikiaji mtu unayemwamini tu na uondoe ufikiaji ukishaisha kuhitajika.
3. Kadi, Link za RSVP, na QR za Kuingia
Kadi zilizohifadhiwa, link za RSVP, QR za wageni, link za scanner, na ripoti hutolewa kulingana na kifurushi, subscription, au event pass uliyonayo. Baadhi ya vipengele vinaweza kuwa na kikomo cha idadi ya kadi, muda wa tukio, idadi ya wageni wa QR, link za scanner, au export.
- Link za RSVP huruhusu wageni kutuma majibu ya mahudhurio na ujumbe.
- QR access humruhusu mwenye tukio kutengeneza pasi za kuingia na kuscan wageni mlangoni.
- Link za scanner zinakusudiwa kwa wafanyakazi wa tukio unaowaamini na zinaweza kuzimwa au kuwekewa muda.
4. Rasimu, Kufuta, na Kurejesha
Rasimu za kadi za mwaliko ni nakala za muda zilizounganishwa na akaunti yako. Rasimu hubaki kufikika kwa siku 7 tangu ilipohifadhiwa mwisho. Rasimu zilizofutwa pia zinaweza kurejeshwa kwa siku 7 tangu zilipofutwa.
Baada ya dirisha la siku 7 la kurejesha, rasimu na rasimu zilizofutwa zinaweza kufichwa na kutoweza kufikika. Baada ya siku 14, zinaweza kufutwa kabisa kwenye database yetu. Rasimu zilizoisha muda, zilizofichwa, au zilizofutwa kabisa hazistahili kurejeshwa au kurejeshewa pesa.
Sera hii ya kusafisha rasimu haiondoi salio la credits za vifurushi binafsi kwenye akaunti yako. Ikiwa rasimu ya kulipia itaisha muda au kufutwa kabisa kabla credit husika haijatumika, salio la kifurushi hubaki hadi litumike au liishe muda kulingana na sheria za kifurushi hicho.
5. Malipo na Vifurushi
Vifurushi vya kulipia hufungua vipengele na vikomo vilivyoonyeshwa wakati wa checkout. Vifurushi vya subscription hujirudia kulingana na mzunguko wa malipo uliochaguliwa. Event pass za mara moja hutumika kwa tukio husika kwa muda au kikomo kilichowekwa.
Checkout na hali ya malipo huchakatwa kupitia Sayari Payments. Ufikiaji, credits, subscriptions, na manunuzi hufunguliwa tu baada ya malipo kuthibitishwa na Sayari Payments kupitia status API au callback iliyosainiwa.
Vikomo vya kifurushi, ikiwa ni pamoja na kadi, wapokeaji, SMS, WhatsApp, link za RSVP, wageni wa QR, link za scanner, exports, na muda wa matumizi, hupungua huduma husika inapotumika. Ukifikia kikomo unaweza kuhitaji kununua kifurushi kingine au kuboresha mpango kabla ya kuendelea.
Mfano, ukinunua kifurushi binafsi cha credits 20 za kadi na ukatumia 5, credits 15 zilizobaki zitaendelea kupatikana baada ya kushusha mpango hadi zitumike au ziishe muda. Ikiwa ulitengeneza kadi kwa kutumia subscription isiyo na kikomo, kadi hizo zilizohifadhiwa zitabaki kufikika baada ya kushusha mpango, lakini uwezo wa subscription ambao haujatumika utaondolewa na vikomo vya Starter vitatumika kwa matumizi mapya.
Kwa ujumla, manunuzi hayarejeshewi pesa baada ya ufikiaji, credits, dispatch, violezo, QR passes, link za RSVP, au faida nyingine za kifurushi kutolewa au kutumika, isipokuwa sheria inayotumika itake vinginevyo.
6. Matumizi Yanayokubalika
Usitumie Sayari E-card kutuma maudhui ya matusi, upotoshaji, uvunjaji wa sheria, udanganyifu, unyanyasaji, au yasiyoidhinishwa. Usipakie maudhui yanayokiuka haki, faragha, au mali ya kiakili ya mtu mwingine.
7. Kusimamishwa na Utekelezaji
Tukigundua matumizi mabaya, ukiukaji wa sera, udanganyifu, maudhui hatarishi, unyanyasaji kwa wageni, au shughuli inayoweza kuathiri Sayari E-card au watumiaji wake, wasimamizi wa Sayari wanaweza kusimamisha mtumiaji, designer, au ufikiaji wa akaunti husika. Kusimamishwa kunaweza kuzuia kutengeneza kadi, kuwasilisha violezo, kutuma dispatch, kutumia RSVP/QR, au kufikia dashboards. Kwa kadri sheria na sera za uhifadhi zinavyoruhusu, akaunti zilizosimamishwa zinaweza kukaguliwa, kurejeshwa, au kufutwa kabisa baada ya kipindi cha kusimamishwa.
8. Violezo na Maudhui ya Designer
Violezo vinavyowasilishwa na designers vinaweza kukaguliwa, kuidhinishwa, kukataliwa, kuondolewa kwenye public, au kufutwa na wasimamizi wa Sayari. Designers wanapaswa kuwasilisha kazi zao halisi au zilizo na leseni sahihi tu.
9. Upatikanaji wa Huduma
Tunajitahidi kuhakikisha Sayari E-card inafanya kazi vizuri, lakini hatuwezi kuhakikisha huduma haitakatika wakati wote. Intaneti, third-party providers, gateways za SMS/WhatsApp, huduma za email, hosting providers, na ruhusa za kamera ya kifaa vinaweza kuathiri upatikanaji.
10. Mabadiliko ya Masharti Haya
Tunaweza kusasisha masharti haya kadri bidhaa inavyokua. Kuendelea kutumia Sayari E-card baada ya masasisho kunamaanisha umekubali toleo la karibuni.
Ilisasishwa mwisho: Agosti 26, 2026